Jumatano, 13 Novemba 2013

TUMBO MAKUFULI WORKSHOP



HISTORIA YA KIWANDA KWA UFUPI

Tumbo Makufuli Workshop(TMW) ni kiwanda cha mtu binafsi kilicho sajiliwa na kuanza kazi mwaka 1982,kwa hatua za awali kilikuwa kiwanda kidogo kinachotoa huduma kwa watu wachache wanao kizunguuka na hasa kilijihusisha na utengenezaji wa funguo za aina zote, lakini kimekuwa na mabadiliko makubwa yanayoendana na mabadiliko ya technologia na sayansi,kwani mpaka sasa kiwanda kinauwezo wa kutengeneza mashine za kusaga unga,mashine za kukoboa mahindi na mpunga,mashine za kukamua mafuta,mashine za kusaga karanga za umeme zenye uwezo wa kusaga gunia moja kwa siku,pia kiwanda kinauwezo wa kumould au kufyatua kifaa chochota cha chuma kilicho vunjika,kwa kuyeyusha vyuma na kuunda kingine kama kile kilicho vunjika,si hayo tu pia kiwanda kinatengeneza mageti ya aina zote,ma safe ya kutunzia fedha,strong rooms kwenye mabenki na mengine mengi kuyaolodhesha hapa


kiwanda kilianzishwa na mzee kabona tumbo maarufu kama tumbo makufuli, na ilikuwa baada ya kuacha kazi shilika la reli TRC wakati huo,hivyo ni fundi mwenye uzoefu wa muda mrefu.kwa sasa kiwanda kinaendelea na utendaji wake katika mkoa wa tabora ambapo apo ndio makao makuu, kwa kupanua wigo wa utoaji huduma kama kiwanda kimeweka mawakala wake kwenye mikoa jilani kama mwanza,shinyanga na kilimanjaro, kwani kiwanda kina ndoto za kutoa  huduma zake Tanzania nzima

CHANGAMOTO WANAZOKABILIANA NAZO VIJANA KATIKA UANZISHAJI WA MIRADI NA SULUHISHO LAKE

Kwa mda mrefu changamoto ya vijana ni mtaji, na hata mwenye mtaji hajui nini afanye. Wengi imepelekea kuishia kumaliza mitaji yao...