Jumatano, 28 Agosti 2024

CHANGAMOTO WANAZOKABILIANA NAZO VIJANA KATIKA UANZISHAJI WA MIRADI NA SULUHISHO LAKE

Kwa mda mrefu changamoto ya vijana ni mtaji, na hata mwenye mtaji hajui nini afanye. Wengi imepelekea kuishia kumaliza mitaji yao na kurudi vijiweni. Imedhaniwa na vijana wengi kwa sababu ya kukosa miongozo au washauri au watu wa kuwashika mikono katika njia zao za mafanikio kuwa kuuza nguo, au viatu au cd, au wigi za wakina mama na nyingine za kufanana na hizo ndo kazi zenye pesa. Mwisho wa siku matokeo huwa tofauti na nguo kujaa vumbi, maana wauzaji wamekuwa wengi. Katika haya maisha cha msingi sana ili kupata pesa na mafanikio yoyote, 1. Ujulikane mpaka watu waku- rebel. Vijana rudia kuisoma hii point uielewe vyema. Kwenye ishu yoyote unatakiwa kukomaa, kung'ang'ania kiasi cha kuhakikisha unajulikana kwa lile unalolifanya. Hili sio zoezi la siku au miezi, hili ni zoezi la mwaka au miaka wakati mwingine. Sio leo unauza cd, kesho unauza soda. 2. Fanya tofauti. Kila ulifanyalo fanya tofauti na namna jamii imezoea au wengine wafanyavyo. Kama unauza mchele, mfungashie na chumvi kijiko kimoja. Watu hawatanunua mchele mtupu na wakwako una chumvi 3. Usiiache biashara yako ijiendeshe. Usiwe mfanyabiashara wa kungoja mteja, pambana kwa mbinu mbalimbali kumvuta mteja, toka nje ya duka kumfata mteja, mbinuka, mjulie hali mteja wako mkubwa akikosekana siku moja, toa huduma ya kuwapelekea wateja bidhaa nyumbani. Pamoja na mbinu izo biashara ya maduka imekuwa kubwa kila kona maduka yamejaa, kwanini usifikilie kuanzisha viwanda vidogo vidogo, ambapo wengi bado hawajawazia, miongoni mwa viwanda vidogo vidogo ni pamoja na:- 1. Mashine za kusaga peanut butter. Hii haiitaji mtaji mkubwa sana kuanza. Ili kiwanda kidogo kikamilike, kunahitajika uwe na mashine ya kukaanga, mashine ya kukoboa karanga zilizokaangwa na mashine ya kusaga karanga. Kiasi cha tsh 4,500,000/= kina tosha kupata mashine zote. Hii biashara inahitajika kufanywa kwanza kwa kutoa huduma kwa wateja wa kila siku wanaosaga kilo 1, 5, 10...nk, lakini pili kwa kusaga karanga zako mwenyewe kwa ajili ya kufungasha ( packing ). Wateja ni shule za kindergarten, shule za boarding, supermarkets, masoko makuu na wateja wadogo wadogo. MASHINE YA KUSAGA PEANUT BUTTER YA UMEME
Hizi ni mashine zinazotumia umeme wa nyumbani yaani single phase. Mashine ya kusaga karanga inasaga mpaka kilo 24 kwa unit moja ya umeme. Ambapo tanesco wanauza unit tsh 400, mfano ukisaga kilo tsh 200 inamaana utapata tsh 4800 kwa unit, faida 4400, ukisagia kilo tsh 300 utapata 7200 faida 6800/= kwa unit.
Ili kuharakisha na kuendana na ukuaji wa soko utatakiwa uwe na mashine ya kukoboa, (picha yake apo juu) hii hutoa vile viganda laini baada ya kukaangwa. Mashine nyingine yenye umuhimu sana ni mashine ya kukaanga. Gharama kwa mashine moja moja kuinunua ni kama ifuatavyo:- 1. YA KUSAGA 1,500,000/= 2. YA KUKOBOA NA KUPETA TSH 1,500,000/= 3. YA KUKAANGA KILO 10 TSH 1,500,000/= JUMLA TSH 4,500,000/= Watengenezaji wazuri wa mashine izo ni T.G.M DESIGNER, Ni kiwanda kidogo sana jiji mwanza ila wanaumakini mkubwa katika kutengeneza mashine bora na imara, wanaushauri mzuri pia na wana guarantee, kwa kipindi flani mashine inakuwa chini yao. Kitu ambacho hauwezi pata toka viwanda vingine. Wanajua capacity ya mota inayohitajika kwa kila mashine Wanatarajia kuanzisha mradi darasa ambapo wateja wao watakaribishwa kujifunza na kuona wigo wa faida, changamoto na namna ya kukabiliana nazo. Tembelea @tumbo51 tiktok, T.G.M designer Facebook, tumbokabona Instagram, T.G.M designer WhatsApp Unaweza wasiliana nao kwa sim 0683628498 au 0679128498 ..........itaendelea part two kiwanda kidogo tofauti ambacho hautajutia kuwa nacho

Maoni 1 :

  1. Kwa iyo mradi ni mmoja tu wa kufanya na ukapata pesa,?

    JibuFuta

CHANGAMOTO WANAZOKABILIANA NAZO VIJANA KATIKA UANZISHAJI WA MIRADI NA SULUHISHO LAKE

Kwa mda mrefu changamoto ya vijana ni mtaji, na hata mwenye mtaji hajui nini afanye. Wengi imepelekea kuishia kumaliza mitaji yao...