Jumanne, 4 Desemba 2018

UTAMBULISHO WA TAWI JIPYA MWANZA

T.G.M DESIGNER ni kifupi cha Tumbo General Machine Designer. Hili ni jina la kiwanda au tawi jipya la kiwanda mwanza. Baada ya kiwanda mama Tabora kinachoitwa T.M.W yaani Tumbo Makufuli Workshop sasa kimezaa tawi mwanza T.G.M Designer. Kiwanda kinapatikana ilemela karibu na PP HOTEL. Tunajihusisha na kazi zote kama zinazofanywa na kiwanda mama Tabora

NEMBO

Slogan yetu ni " your life simplified with our makes" yaani maisha yako yanarahisishwa na tunavyounda. Na ili yarahisishe lazima uwe tayali kama mteja kututyma kazi. Na ili ututume lazima tuwe wakweli, wapole, wastaarabu, wanyenyekevu na ubora wa kazi zetu. Na haya ndio malengo na maisha tuliyochagua na wateja wetu. Kwa chochote ambacho utahudumiwa visivyo usisite kuwasiliana nasi nakusema wazi. Maana amna mkamilifu duniani.

NEMBO KWA KIWANDA CHA TABORA

Jumapili, 28 Januari 2018

UTARATIBU MPYA WA UUZAJI BIDHAA ZETU KWA WATEJA WA MBALI

Tumekuwa na matangazo mengi online juu ya bidhaa zetu, matangazo tumeweka what'sapp, facebook, twitter, instagram, zoomtanzania, kupatana, na, tumbomakufuli.blogspot.com, sasa tumekuwa na wateja wengi online kuliko wanaotufikia kiwandani kwetu. Hii inaleta haja ya kuboresha njia ya biashara kimtandao  kuifanya bora na salama kwa mteja na kwetu pia.
tunajinsi mbili za kufanya biashara hii ni uchaguzi wako mteja juu ya njia ipi utaona salama kupata bidhaa yako.

NJIA YA KWANZA
Ukipendezwa na bidhaa yetu kwanza waasiliana nasi kujua kama ipo, na kutoa vigezo ambavyo wewe unahitaji, vikiwiana na ukawa na utayali wa kununua, nenda kwenye ofisi za usafirishaji unazozijua na kuziamini kama ni mabasi au image power, wakuunganishe na wakala wao au ofisi yao iliyopo tulipo sisi kama kiwanda. kwa sasa tupo mwanza kama branch, na target market. ingawa makao makuu yapo Tabora lakini bidhaa zote huletwa mwanza kwa mauzo. kwa iyo watakuunganisha na wakala wa mwanza, utampa vigezo unavyotaka vya bidhaa husika. mimi ntapeleka bidhaa hiyo kwa wakala au ofisi ya usafirishaji utanipa jina la huyo uliemuomba ubalozi, ntamuonyesha tutatest mbele yake akilidhika atakukikishia kuwaa kila kitu kipo sawa na wewe utanitumia pesa ya kununulia bidhaa hiyo ntaiacha hiyo biddhaa hapo ofisini kwa usafirishwaji

NJIA YA PILI
Hii inapendeza kwa wateja ambao tulishafanya biashara mara ya kwanza au atakama anaanza biashara na sisi kwa mara ya kwanza ila amepewa ushuhuda kwa mteja wetu ambaye tulishafanya biashara nae
ambapo mteja ataulizia bidhaa aitakayo kama ipo, na kama ipo atatakiwa kutuma hela moja kwa moja kwangu na hatua zaidi zitafuata

Nje ya taratibu hizi TUMBO MAKUFULI WORKSHOP haitajiingi kwenye biashara yoyote na wateja wa mbali au wamitandaoni

ASANTENI NA KARIBUNI SANA

CHANGAMOTO WANAZOKABILIANA NAZO VIJANA KATIKA UANZISHAJI WA MIRADI NA SULUHISHO LAKE

Kwa mda mrefu changamoto ya vijana ni mtaji, na hata mwenye mtaji hajui nini afanye. Wengi imepelekea kuishia kumaliza mitaji yao...