Jumatatu, 21 Agosti 2017

muendelezo : MRADI WA KUSAGA KARANGA KUWA NTWILI


MRADI WA MASHINE YA KUSAGA KARANGA KUWA NTWILI
Katika historia ya usagaji karanga, wazee wetu kwenye karne ya kumi na tisa walikuwa wanasaga kwenye mawe. Ambapo kunajiwe kubwa na dogo ambalo ndo anapitisha juu ya karanga ambazo zinakuwa kati ya jiwe dogo na kubwa na kusugua kwa mikono miwili.
Baadae waliboresha wakatengeneza ubao unaoitwa mbehe na msiginio hivi Vilikuwa vya mbao,  lakini bado ufanisi ulitosheleza maisha ya kipindi chao.  Kwa sasa kumekuwa na gunduzi mbalimbali za Mashine za kusagia karanga ambazo zimekuwa ni bora kuliko hizo nilizoeleza hapo juu. Zimeundwa kwa chuma husaga kwa uharaka zaidi. Zipo za mkono



Na zipo za umeme, ila hizi za umeme ni maalum kwa biashara,   yaani unasaga ili uuze karanga Kama bidhaa.

KWA NINI USAGAJI WA KARANGA NAO UMEKUWA MRADI
usagaji  wa Karanga Umekuwa mradi kutokana na sababu nyingi sana;
1. Wingi wa majukumu kwa wahitaji. Wahitaji wengi wa karanga iliyosagwa wanabanwa na majukumu aidha ya kiofisi au ata ya nyumbani kiasi kwamba kupata mda wa kusaga karanga kwa matumizi yake anaona uzito. Hivyo kutoa nafasi kwa wengine kuuza madukani hizi karanga.
2. Upatikanaji wa karanga sehemu flani kuliko sehemu nyingine; mfano Tabora inasifika sana kwa Karanga hasa wilaya ya urambo, lakini Arusha ni adimu, hivyo wenyekuzijua fulsa wanasaga Karanga nakuzisafirisha mikoa ambayo kunauadimu.
3. Uhitaji wa utofauti kati ya mtu na mtu katika kuanzisha miradi. Ile hali ya kutaka kuwa tofauti kati ya wadau, huchochea mtu kufikilia zaidi na kufikia katika kuanzisha miradi ambayo huwa na Matokeo mazuri. Na hapo watu wakaanzisha mashine hizi ili kuwa tofauti.

NAMNA YA UENDESHAJI WA MRADI WA USAGAJI WA KARANGA.
Kwanza ni lazima ulijue soko lako. Na liwe la uhakika, hii ujulikana kwa kufanya tafiti za soko (marketing research). Ukijua lilipo soko jua unahitajika kuandaa bidhaa yako.

Kutegemea na kiwango cha uhitaji wa wateja wako, unaweza anza na mashine za mkono ambazo nikubwa. Zinauzwa tsh 80,000/=. Ambapo mtengenezaji na msambazaji mkubwa ni Tumbo Makufuli Workshop wa Tabora. Ambao unaweza kuwapata kwa simu no +255683628498, unaweza nunua mashine mbili za mikino ili uendane na wateja wako.

Kama uhitaji ni mkubwa Sana,  unaweza nunua mashine ya kusaga karanga ya umeme . Pia Mafundi na wasambazaji ni haohao Tumbo Makufuli Workshop. Bei ya mashine hii ni tsh 1000,000/= inauwezo wa kusaga gunia moja na nusu kwa siku. Sasa kwa hii mashine unakuwa na kiwanda kamili.

Baada ya usagaji Unatakiwa kuwa na vifungashio vyenye muonekano mzuri na safi. Hii itakufanya uweze kuuza mpaka kwenye supermarkets mbalimbali. Package nzuri na brand name yako pia itakupa umaarufu.

Pia katika misingi ile ile ya kuleta utofauti, Kama mtakumbuka huko nyuma tulizungumzia hili,   unaweza kuzarisha bidhaa zote zitokanazo na Karanga,  mfano mafuta ya karanga, pinnate butter , mashudu ya Karanga kwa ajili ya mifugo. Karanga za kutafuna za kawaida na za mayai. Kwa hili lazima uwe na duka kamili kwa bidhaa zako tu,  uwe na brand yako ambayo inazingatia ubora na viwango.

WAPI WATEJA WANAPATIKANA
soko la Karanga ni kubwa sana, kwa hapa kwetu jamii nyingi zimekuwa zinatumia Karanga kama kiungo kwenye mboga au chakula cha watoto,  pia karanga zimechukua nafasi ya Jojo tangu pale zilipogundulika athari za Jojo mwilini  mwetu.  Hivyo ata eneo ulipo wateja wapo.
Lakini pia nchi jirani kama Malawi wanauhitaji mkubwa wa hii bidhaa ya karanga.
Lakini Kama haitoshi,  kuna mikoa ambayo inauhaba wa karanga kutokana na ukweli kwamba wao hawalimi karanga,  napo nisehemu muhimu kupeleka bidhaa hii.

Itaendelea tena wakati mwingine. Usisite kutoa maoni yako na kujiunga nasi ili uweze kupata mwanga na baadae kuwa na uhakika wa nini cha kufanya

Jumanne, 1 Agosti 2017

muendelezo wa MIRADI YENYE GHARAMA NDOGO YA UENDESHAJI LAKINI FAIDA KUBWA.


MRADI WA KUFYATUA TOFARI

Ukuaji wa mji unategemea sana Ukuaji wa sekta ya ujenzi, kila mmoja anawaza kujenga kama sio nyumba basi Itakuwa fensi kuzunguruka nyumba. Limekuwa hitaji la muhimu sana kwa wateja kupata tofari kwa haraka,  tofari imara na nzuri.  Kumbe ukiwa na mashine yenye uwezo mzuri na ukatengeneza Tofari lenye sifa wateja wanahitaji unaweza tajilika kwa kasi ya ajabu.

MASHINE YA KUFYATULIA TOFARI
Kwa sababu ya kasi ya uhitaji wa wateja, ni vyema kutumia mashine ya  kufyatua ya umeme,  ambayo itaendana na kasi ya uhitaji wa wateja.
Mashine hii ya umeme kwa siku nzima inauwezo wa kufyatua TOFARI 1300,
Hivyo kwa kuwa inahusika katika kazi ngumu sana lazima iwe imeundwa kwa vyuma imara  ili kuruhusu uzarishaji huo.

VITU VYA MUHIMU KUZINGATIA KATIKA UTEKELEZAJI WA MRADI HUU

1. RATIO YA CEMENT KWENYE UDONGO
Wengi huitaji faida kubwa hivyo kuweka uwiano mdogo kati ya cement na mchanga,  kupelekea biashara kuwa ngumu na kukaribisha sifa mbaya kwenye biashara hii,  hivyo kuwaharibia wale wanaotengeneza kiusahihi. Ratio nzuri na bora ni Tofari 40 kwenye mfuko au Tofari 45 kwa mfuko,  sasa unakuta mtu anatoa Tofari 50 kwenye mfuko kiasi kwamba mchanga na cement havishikani,  ukipitisha kidole kwa kukandamiza unatoka mchanga. Hii haifai.

2. MUDA WA KU VIBRATE NA KUKANDAMIZA MFUNIKO.
mashine hii ya umeme inakifaa maalum cha kushindilia udongo kwa kutetemesha hivyo sasa operator lazima atumie mda kidogo kutetemesha ili udongo ushikane Vinginevyo hautashikana na kupelekea kutoa Tofari lisilo imara. Pamoja na hilo lazima ukandamizaji wa mfuniko wa juu uendane na utetemeshaji wa Mashine.

3. MADINI YALIYOMO KWENYE MCHANGA  WA KUFYATULIA.
Kuna baadhi ya madini ambayo si rafiki na Cement, ata ukiweka ratio ya 10 lakini Tofari bado lingetoka sio imara,  hivyo ni muhimu kuchunguza content ya mchanga kabla haujaanza uzarishaji. Madini kama chumvi (NaCl) si rafiki na cement kabisa huzidisha unyevu na kupelekea cement kuishiwa nguvu yake kutokana na reaction kati yao.

4. UMWAGILIZIAJI WA MAJI MDA MCHACHE BAADA YA UFYATUAJI
Uimara wa Tofari lililozingatia vigezo vingine vyote hapo juu unategemea umwagiliaji wa maji.  Tofari imara linahitaji maji mengi baada ya kufyatuliwa.

BEI YA TOFARI
Wengi wanauza 1000/= lakini hawajawa wazi kwa ratio ipi?  Sasa kwa lengo la kuleta utofauti unaweza kufyatua TOFARI zenye ratio tofauti tofauti na bei ikawa tofauti. Mfano ratio ya 40 ukauza 1300/= na usafiri, 1200/= bila usafiri,  ratio ya 45 ukauza tsha 1100/= na usafiri, 1000/= bila usafiri.
Kumbe kwa uwezo wa kuzarisha Tofari 1300 kwa siku, utaingiza tsh 1,300,000/=, kwa idadi hii unauhakika wa kupata faida ya tsh 300,000/=.
Itaendelea wakati mwingine endelea kutufatilia ujue zaidi 

CHANGAMOTO WANAZOKABILIANA NAZO VIJANA KATIKA UANZISHAJI WA MIRADI NA SULUHISHO LAKE

Kwa mda mrefu changamoto ya vijana ni mtaji, na hata mwenye mtaji hajui nini afanye. Wengi imepelekea kuishia kumaliza mitaji yao...