Jumatano, 26 Julai 2017

muendelezo: MIRADI YENYE GHARAMA NDOGO YA UENDESHAJI LAKINI FAIDA KUBWA.

Kipindi kilichopita tuliishia kwenye mradi wa Mashine ya kusaga na kukoboa nafaka. Ambapo leo tunaendelea na mapato inayoweza kupata kwa siku, pamoja na kujadili miradi mingine. Karibu.

MAPATO KWA SIKU
Kama unatoa huduma kwa wakazi wa jirani na mashine tu,  kusaga na kukoboa kwa siku unaweza ingiza kati ya tsh 90000/= mpaka 100000/= eneo ulipoweka mashine kuna population kubwa

Kama unatoa huduma kwa wakazi wa jirani na mashine pamoja na kusaga unga wa kufunga kwenye viroba kwa siku  unaweza ingiza kati ya tsh laki moja na nusu mpaka tatu.

WAPI UNAWEZA PATA MASHINE HIZI KWA HARAKA
Kwa sasa viwanda vingi vinatengeneza mashine hizi,  hivyo unaweza pata kokote kwa hapa Tanzania,  ila unapohitaji Mashine bora na imara ambayo itafikia vigezo tulivyotaja hapo juu, ni TUMBO MAKUFULI WORKSHOP pekee ambao wamebaki na sifa ya Kutengeneza bidhaa bora na imara. Wanapatikana Tabora Mjini,  kwa namba +255683628498 au +255757027691 au email: tumbokabona@gmail.com

2. MRADI WA KUCHANA MBAO KWA BENSAW
Bensaw ni mashine ya kuchana mbao yenye msumeno mwembamba uliopinda,  ni tofauti na mashine ya kuchana kwa msumeno wa duara.
Add BENSAW MACHINE. 


TOFAUTI KATI YA BENSAW NA MASHINE ZINGINE ZA KUCHANA MBAO
Bensaw inauwezo wa kuchana gogo lenye mduara wa kipenyo cha mpaka futi 2 au inch 24 wakati mashine zingine zinaweza kuchana gogo lenye mduara wa kipenyo cha mpaka futi 0.5 au inch 6 ambapo gogo mpaka ligeuzwe ili kutoa ubao au banzi lenye upana wa inch 12,  wakati mwingine njia hukosana, yaani ulipopita msumeno wa chini unakosana na utakaopita juu ili utoe banzi au ubao, hivyo kuacha kazi chafu isiyofurahisha Mteja

Tofauti nyingine ni muda wa utendaji,  kwa bensaw huchukua muda mfupi sana kutimiza kazi ambayo  mashine zingine zingefanya kwa muda wa mpaka mara tatu au nne ya muda huo

Bensaw huacha kazi safi sana ukilinganisha na mashine zingine

MAPATO YA SIKU YA BENSAW
Kwa siku unaweza ingiza kati ya tsh 100,000/= mpaka 200,000/= cha msingi ni kuweka Mashine kwenye maeneo ambayo kuna wakulima wa miti au mapori makubwa,  mfano unaweza kuweka Tabora Mjini au Mwanza,  sengelema, au mpanda.

NAMNA YA KULETA UTOFAUTI
Pamoja na huduma ya kuchana mbao kwa wateja wako,  unaweza kuanzisha unit yako inayoenda polini kuleta magogo wakati huo pia unanunua toka kwa watu baki kisha unachana mbao na Kusafirisha mikoani kama Dar-es-salaam au Mwanza.

Bado pia ukaweka unit nyingine ya Mafundi ambao wanatengeneza fenicha mbalimbali, kama kabati za kisasa, meza na viti pamoja na top za milango yenye muonekano wa kisasa na Kusafirisha kwenye miji mikubwa.

Pia maranda yanayotokana na uchanaji wa mbao unaweza tengeneza nishati mbadala ya kupikia badala ya kuyatupa,  na hivyo kujiongezea kipato

MAMBO YA KUZINGATIA KWENYE MRADI HUU

1. kuwa na vibari vya kuvuna maliasili kama hizo mbao. Vinginevyo utaiona chungu na haifai
2. Kwa kuanzia unaweza kufanya bila kulipa mapato TRA kwa kuwa unaanza, ila biashara  ikishamili lazima uakikishe kaisali anapata fungu lake.
3. Kutafuta eneo kubwa la kufanyia kazi,  maana wateja watakuja na magari yao yamepakia magogo, lazima eneo la kuweka magogo yao liwe kubwa na salama

BEI YA MASHINE YA BENSAW
mashine ya bensaw kwa sasa original inauzwa mpaka Milioni tisa bila mota. Inakuwa katika material ya dongo ambayo sikushauri kuwa na mashine yenye material haya kwani ni rahisi kuvunjika.
Tumbo MAKUFULI workshop wanatengeneza Mashine hiyohiyo kwa material ya chuma kwa tsh 6,500,000/=.



Itaendelea wakati mwingine endelea kutufatilia ujue zaidi, usisahau kutufollow apo chini na kuacha comment yako.  

WRONG WAY FOR INDUSTRIAL CHANGE IN AFRICA

Wrong way always end up  to wrong destinations, that may result to culture shock, this is what Africa industrialization process reach.
Changes to be effective should be gradual, this to give room for adapting it, and giving yourself chance to fix some of challenges which are always accompanied with changes to fit your life style, but also to evaluate the benefit of changes to your society. There are many reasons to why changes should be gradual, but my focus to write this is to spark the view on wrong way that Africa choose toward industrialization.

The history of industrialization is clear, industrialization was spearheaded with innovations and discovery, whereas small scale discoveries were change to large beneficial projects. The spirit of innovation and discovery is discouraged in Africa this is clear via a couple of examples, in Africa if a person discover a gun for example will be considered as wrong doer and strong measures will be taken upon him or her by the government.  In Mbeya region, in Tanzania there was a youth who was able to make an aeroplane, but the government was deef and brind on that,  till the external countries saw him and take him for training purposes.

When you hear about industrial change in African countries, we are focusing on initiate industries 99% with technology from abroad. Local industries are not know,  they seem as doing their day to day activities for subsistence only.

Wonderful enough, is that African governments are calm on success of internal industrial,  but external countries are fighting hard to take us from one stage to another of development, it is now wise for associations which focus to develop African local industries to go direct to those local industries otherwise  they would encounter some middlemen who may interrupt the benefits which are intended to local industries in a way that it may reach reduced or nothing.

Will continue soon.

MIRADI YENYE GHARAMA NDOGO YA UENDESHAJI LAKINI FAIDA KUBWA

    Watu wengi wenye pesa hushindwa au huwa na wakati mgumu katika kufikilia au kuanzisha miradi yenye faida kubwa,  ambapo hubaki kuigiliziana kupelekea wigo wa mapato kuwa mdogo sana kiasi cha kujihusisha na ushirikina wakizani ndio itakuwa njia sahihi ya kupambana na ushindani na kujipatia wateja wengi,  kitu ambacho huwa ni tofauti.

Katika biashara hasa unapotaka kuanzisha mradi mpya usifikili sana kitu kipya ambacho hakipo, kwani itawachukua mda mrefu wateja kuzoea na kuona umuhimu wa biashara hiyo kwao,  lakini pia ukifanikiwa wengine wenye pesa wataiga na kuanza kukuletea changamoto za ushindani.  na inauma sand pale unapojua wewe ndio muasisi wa fikra, labda ukisha fanikiwa uende ukaisajili COSOTA upate umiliki wa aidia yako na yoyote atakaeingia utamshtaki,  lakini nayo ni ghari sana, na inahitaji mda pia.
 
Cha msingi cha kufanya ni kubaki katika ile ile miradi ya zamani ambayo wengi wanafanya ila wewe utafute utofauti wake ili kuendana na ushindani.

MIRADI YENYE FAIDA KUBWA ZAIDI

1. MASHINE YA KUKOBOA NA KUSAGA UNGA.
Huu ni mradi maarufu sana na asilimia kubwa sana ya wenye pesa wanafanya mradi huu. Lakini kama nilivyokwisha sema hapo juu : ni vyema kujihusisha na miradi ambayo wengi wanafanya kuliko kuanzisha mradi mpya cha, msingi ni kuweka utofauti tu.
Mashine ya kusaga No.  35 inauzwa tsh 800,000/=,  kwa kuanzia unaweza kununua hii mashine kwanza ila badae ukikomaa kibiashara unaweza kununua mashine nyingine aina ya LB7 AU LB4  ambazo bei yake ina range kati Milioni moja na mbili,  ila uzalishaji wake unakuwa mkubwa zaidi ya NO. 35 au 50. Gharama za kuunganisha umeme ni tsh 400,000/=, mota moja inauzwa tsh  1200000/= mpaka 1500000/=

Unaweza toa huduma ya kusaga kwa wateja wadogo wadogo, ambayo ndio kawaida,  lakini pia ukasaga kwa ajili ya kufunga unga kwenye viroba na kuuza kwenye maduka ya jumla na rejareja pia, maana yake unakuwa na bland yako.
Bado pia pumba ni bidhaa adimu sana na inahitajika sana kwa wafugaji. Mikoa kama Tabora pumba inabei rahisi sana lakini mikoa kama Mwanza,  Arusha na Kilimanjaro pumba inabei sana,  usafirishaji kwa gunia ina range kwenye 3000/= mpaka 5000/=.

Bado pia mashine hizo hizo unaweza kusaga chakula cha kuku na ukakifunga kwa ujazo maalum, cha msingi sana kwenye chakula cha kuku ni kuakikisha unaweka content zote muhimu,  yaani virutubisho muhimu uakikishe vimo Vinginevyo wateja watakukimbia.
Mpaka hapo utakuwa tofauti na wengine wengi wenyekutoa huduma sawa na wewe.

SIFA YA KINU IMARA
1. Kinu imara kinatakiwa kuundwa kwa kutumia plain ion sheet yenye unene wa millimeter kuanzia 5 mpaka 8, ili kuepuka kutoboka au kwisha haraka
2. Feni kubwa kwa uwiano na size ya kinu ili kuharakisha usafirishaji wa unga toka kwenye kinu mpaka kwenye mfuko
3. Beseni kubwa linaloruhusu kuweka mzigo mwingi kwa wakati mmoja.

Itaendelea wakati mwingine endelea kutufatilia ujue zaidi juu ya miradi yenye faida kubwa zaidi.

Jumamosi, 15 Julai 2017

UYEYUSHAJI NA UMIMINAJI WA VYUMA

Ni hatua ya kimapinduzi ambayo Tumbo Makufuli workshop wameifikia kwa sasa ambapo  chuma aina ya aluminum na copper vinaweza kuyeyushwa na kuunda umbo lingine upendalo,
Hii unaweza kuwa na hatua bora na manufaa kwa wateja wetu wengi ambao aidha gari yake, pikipiki yake au kifaa chake chochote kinaweza vunjika na labda spare yake hamna au ni ghari sana basi kuweza kukipata kiurahisi toka Tumbo Makufuli workshop

HATUA ZA UYEYUSHAJI NA UMIMINAJI WA VYUMA
1. kwanza kabisa unatakiwa kuwa na mould au pattern ambayo inasura ya kile unataka kumimina,  mould unaweza kuwa ya udongo au bati jembambamba

2. Kuandaa raw materials ya kutosha kipimo cha kitu unachotaka kumimina,  ambapo utapima uzito wa kile kitu kilichovunjika kisha utapima kiasi cha raw materials sawa au zaidi kidogo ya kipimo halisi kisha utaweka kwenye chungu
Chungu kinaweza kuwa cha chuma kizito au cha madini ya ulanga ambayo uhimili moto

3.Washa moto wako kwa aidha makaa ya mawe,  kuni au mkaa wa kawaida, ila unabidi kuuchochea kwa kutumia browa ili kupandisha joto kwa haraka

4. Kila baada ya mda wa nusu saa chukua thermometer yako na upime joto, maana material tofauti yana boiling point tofauti ukiona joto limefikiwa itakuwa ni ishara kuwa tiyali vimeyeyuka

5. Taratibu fungulia koki ya molten material  kuelekea kwenye pattern yako au nyanyua chungu chote na umimine uji kwenye pattern yako

6. Subili ipoe, kisha vunja pattern yako au pachua pattern yako na utabakiwa na kitu halisi sawa na kile kilivunjika

7. Safisha vizuri na uki polish tayali kwa matumizi

Nitoe wito kwa wateja wetu kuwa sasa huduma hii ya umiminaji inafanyika hapa kwetu Tanzania  na unaweza pata kwa haraka zaidi kupitia sisi
Kuna wale wanatengeneza  sabuni  bila nembo kwa sasa unaweza pata nembo nzuri uipendayo  kwa ajili ya kisambaza bland yako na watu wakujue,  na kujitofautisha

Kwa wahitaji wa huduma hii au bidhaa yoyote wanaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba +255683628498

UMUHIMU WA VIWANDA VIDOGO VIDOGO KATIKA MAISHA YA KILA SIKU.

Viwanda Vidogo Vidogo vimekuwa chachu ya maendeleo ya mtu mmoja mmoja na ata taifa kwa ujumla,  Ingawa mchango wake kwa taifa haujatiliwa maanani

Ni viwanda ambavyo Kimsingi ni kama mayatima  havina mlezi mwenye uhitaji wa Kweli wa kuwatoa, yaani kuwafanikishia matakwa yao hasa ya kukuwa na ata kuwa viwanda vya kati. Waliopo they act as middle man kutafuta kazi kwa jina la flani na kufanya wao kwa mafundi wao kwa manufaa yao. Ufatiliaji wa siku hadi siku wa maendeleo ya viwanda hivyo Kama hamna, wao wanangoja maonyesho na siku kaja mfadhili flani ndo uyawaona na matai na note book kwenye kila kiwanda ata kile cha uchocholoni. Hatutafika hivi. Imebaki juhudi ya fundi mwenye kiwanda kufikia hayo.

MCHANGO WA VIWANDA VIDOGO KATIKA MAENDELEO YA TAIFA
1. Viwanda hivi vinatoa ajila kwa vijana . Ajila inayotolewa ingawa ni ndogo ila inamaslahi makubwa sana katika ustawi wa taifa letu,  vijana ambao labda kwa kukosa cha kufanya wangeweza kuwa wavuta bangi, wizi, ubakaji na mengine mengi ya kufanana na hayo, sasa wanapata kazi ambayo inawaepusha na hayo kwani watakuwa bize na majukumu ya siku kiwandani

2. Upatikanaji wa bidhaa zinazofikia uhitaji wa wateja, viwanda Vidogo Vidogo mara nyingi hujihusisha na utengenezaji wa mashine ndogo ndogo ambazo huwa na ubora na uimara zaidi ya zile zitokazo nje, kwa vyuma ambavyohutumika ni imara na vizito kuliko, hivyo kukidhi haja ya wateja.

3. Kupunguza usumbufu wa kuagiza nje,  viwanda hivi hiweza kubuni Mashine mbalimbali kulingana na uhitaji wa Mteja, tu kwa kuwa wateja wengi hawajajua namna ya kuwatumia hawa Mafundi hapa ndo msukumo wa ubunifu unafia

4. vinasaidia katika mzunguruko wa mitaji.  Hii ni kwa mantiki moja, Fundi akinunua malighafi kwa ajili ya kazi zake ndio wanafanya existence ya maduka haya ya hardware , na ndio mitaji ya hao wenye maduka inakuwa na mzunguruko kufana, ata T. R. A wakizungurukia wanapata pato la taifa, hivyo uchumi wa taifa kukuwa.
Kwa leo tuishie hapo kwa yoyote mwenye Mawazo,  ushauri basi unakaribishwa


Ijumaa, 14 Julai 2017

STAND ZA VIATU

Kwa sasa Tumbo Makufuli workshop tunatengeneza stand za viatu za kijanja ambazo zinaendana na mazingira ya chumba chako na kukifanya cha kijanja na cha kisasa.
Kwa wahitaji warejareja na jumla tuwasiliane kwa simu no 0683628498, bei ni tsh 60000/= kwa rejareja na  50000/= kwa  jumla  

CHANGAMOTO WANAZOKABILIANA NAZO VIJANA KATIKA UANZISHAJI WA MIRADI NA SULUHISHO LAKE

Kwa mda mrefu changamoto ya vijana ni mtaji, na hata mwenye mtaji hajui nini afanye. Wengi imepelekea kuishia kumaliza mitaji yao...