Jumatano, 26 Julai 2017

muendelezo: MIRADI YENYE GHARAMA NDOGO YA UENDESHAJI LAKINI FAIDA KUBWA.

Kipindi kilichopita tuliishia kwenye mradi wa Mashine ya kusaga na kukoboa nafaka. Ambapo leo tunaendelea na mapato inayoweza kupata kwa siku, pamoja na kujadili miradi mingine. Karibu.

MAPATO KWA SIKU
Kama unatoa huduma kwa wakazi wa jirani na mashine tu,  kusaga na kukoboa kwa siku unaweza ingiza kati ya tsh 90000/= mpaka 100000/= eneo ulipoweka mashine kuna population kubwa

Kama unatoa huduma kwa wakazi wa jirani na mashine pamoja na kusaga unga wa kufunga kwenye viroba kwa siku  unaweza ingiza kati ya tsh laki moja na nusu mpaka tatu.

WAPI UNAWEZA PATA MASHINE HIZI KWA HARAKA
Kwa sasa viwanda vingi vinatengeneza mashine hizi,  hivyo unaweza pata kokote kwa hapa Tanzania,  ila unapohitaji Mashine bora na imara ambayo itafikia vigezo tulivyotaja hapo juu, ni TUMBO MAKUFULI WORKSHOP pekee ambao wamebaki na sifa ya Kutengeneza bidhaa bora na imara. Wanapatikana Tabora Mjini,  kwa namba +255683628498 au +255757027691 au email: tumbokabona@gmail.com

2. MRADI WA KUCHANA MBAO KWA BENSAW
Bensaw ni mashine ya kuchana mbao yenye msumeno mwembamba uliopinda,  ni tofauti na mashine ya kuchana kwa msumeno wa duara.
Add BENSAW MACHINE. 


TOFAUTI KATI YA BENSAW NA MASHINE ZINGINE ZA KUCHANA MBAO
Bensaw inauwezo wa kuchana gogo lenye mduara wa kipenyo cha mpaka futi 2 au inch 24 wakati mashine zingine zinaweza kuchana gogo lenye mduara wa kipenyo cha mpaka futi 0.5 au inch 6 ambapo gogo mpaka ligeuzwe ili kutoa ubao au banzi lenye upana wa inch 12,  wakati mwingine njia hukosana, yaani ulipopita msumeno wa chini unakosana na utakaopita juu ili utoe banzi au ubao, hivyo kuacha kazi chafu isiyofurahisha Mteja

Tofauti nyingine ni muda wa utendaji,  kwa bensaw huchukua muda mfupi sana kutimiza kazi ambayo  mashine zingine zingefanya kwa muda wa mpaka mara tatu au nne ya muda huo

Bensaw huacha kazi safi sana ukilinganisha na mashine zingine

MAPATO YA SIKU YA BENSAW
Kwa siku unaweza ingiza kati ya tsh 100,000/= mpaka 200,000/= cha msingi ni kuweka Mashine kwenye maeneo ambayo kuna wakulima wa miti au mapori makubwa,  mfano unaweza kuweka Tabora Mjini au Mwanza,  sengelema, au mpanda.

NAMNA YA KULETA UTOFAUTI
Pamoja na huduma ya kuchana mbao kwa wateja wako,  unaweza kuanzisha unit yako inayoenda polini kuleta magogo wakati huo pia unanunua toka kwa watu baki kisha unachana mbao na Kusafirisha mikoani kama Dar-es-salaam au Mwanza.

Bado pia ukaweka unit nyingine ya Mafundi ambao wanatengeneza fenicha mbalimbali, kama kabati za kisasa, meza na viti pamoja na top za milango yenye muonekano wa kisasa na Kusafirisha kwenye miji mikubwa.

Pia maranda yanayotokana na uchanaji wa mbao unaweza tengeneza nishati mbadala ya kupikia badala ya kuyatupa,  na hivyo kujiongezea kipato

MAMBO YA KUZINGATIA KWENYE MRADI HUU

1. kuwa na vibari vya kuvuna maliasili kama hizo mbao. Vinginevyo utaiona chungu na haifai
2. Kwa kuanzia unaweza kufanya bila kulipa mapato TRA kwa kuwa unaanza, ila biashara  ikishamili lazima uakikishe kaisali anapata fungu lake.
3. Kutafuta eneo kubwa la kufanyia kazi,  maana wateja watakuja na magari yao yamepakia magogo, lazima eneo la kuweka magogo yao liwe kubwa na salama

BEI YA MASHINE YA BENSAW
mashine ya bensaw kwa sasa original inauzwa mpaka Milioni tisa bila mota. Inakuwa katika material ya dongo ambayo sikushauri kuwa na mashine yenye material haya kwani ni rahisi kuvunjika.
Tumbo MAKUFULI workshop wanatengeneza Mashine hiyohiyo kwa material ya chuma kwa tsh 6,500,000/=.



Itaendelea wakati mwingine endelea kutufatilia ujue zaidi, usisahau kutufollow apo chini na kuacha comment yako.  

Maoni 1 :

CHANGAMOTO WANAZOKABILIANA NAZO VIJANA KATIKA UANZISHAJI WA MIRADI NA SULUHISHO LAKE

Kwa mda mrefu changamoto ya vijana ni mtaji, na hata mwenye mtaji hajui nini afanye. Wengi imepelekea kuishia kumaliza mitaji yao...