Jumamosi, 15 Julai 2017

UYEYUSHAJI NA UMIMINAJI WA VYUMA

Ni hatua ya kimapinduzi ambayo Tumbo Makufuli workshop wameifikia kwa sasa ambapo  chuma aina ya aluminum na copper vinaweza kuyeyushwa na kuunda umbo lingine upendalo,
Hii unaweza kuwa na hatua bora na manufaa kwa wateja wetu wengi ambao aidha gari yake, pikipiki yake au kifaa chake chochote kinaweza vunjika na labda spare yake hamna au ni ghari sana basi kuweza kukipata kiurahisi toka Tumbo Makufuli workshop

HATUA ZA UYEYUSHAJI NA UMIMINAJI WA VYUMA
1. kwanza kabisa unatakiwa kuwa na mould au pattern ambayo inasura ya kile unataka kumimina,  mould unaweza kuwa ya udongo au bati jembambamba

2. Kuandaa raw materials ya kutosha kipimo cha kitu unachotaka kumimina,  ambapo utapima uzito wa kile kitu kilichovunjika kisha utapima kiasi cha raw materials sawa au zaidi kidogo ya kipimo halisi kisha utaweka kwenye chungu
Chungu kinaweza kuwa cha chuma kizito au cha madini ya ulanga ambayo uhimili moto

3.Washa moto wako kwa aidha makaa ya mawe,  kuni au mkaa wa kawaida, ila unabidi kuuchochea kwa kutumia browa ili kupandisha joto kwa haraka

4. Kila baada ya mda wa nusu saa chukua thermometer yako na upime joto, maana material tofauti yana boiling point tofauti ukiona joto limefikiwa itakuwa ni ishara kuwa tiyali vimeyeyuka

5. Taratibu fungulia koki ya molten material  kuelekea kwenye pattern yako au nyanyua chungu chote na umimine uji kwenye pattern yako

6. Subili ipoe, kisha vunja pattern yako au pachua pattern yako na utabakiwa na kitu halisi sawa na kile kilivunjika

7. Safisha vizuri na uki polish tayali kwa matumizi

Nitoe wito kwa wateja wetu kuwa sasa huduma hii ya umiminaji inafanyika hapa kwetu Tanzania  na unaweza pata kwa haraka zaidi kupitia sisi
Kuna wale wanatengeneza  sabuni  bila nembo kwa sasa unaweza pata nembo nzuri uipendayo  kwa ajili ya kisambaza bland yako na watu wakujue,  na kujitofautisha

Kwa wahitaji wa huduma hii au bidhaa yoyote wanaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba +255683628498

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

CHANGAMOTO WANAZOKABILIANA NAZO VIJANA KATIKA UANZISHAJI WA MIRADI NA SULUHISHO LAKE

Kwa mda mrefu changamoto ya vijana ni mtaji, na hata mwenye mtaji hajui nini afanye. Wengi imepelekea kuishia kumaliza mitaji yao...